Africa Kids Book Club

WEMA HAUOZI

Wema ni haki ya kuwasaidia watu na majirani. Kamakumsaidia mgonjwa hospitalini au kumwelezea mwanafunzi majibu,yaonyesha kuwa na wema hupeleka mtu mbali maishani. 

Babu na nyanya yetu hutueleza kwamba ukiwa na wema hutapatana na shinda. Msemo huu una ukweli. Mfano,kuna mwanafunzi mmoja katika darasa letu, jina lake ni Juma ana umri wa miaka kumi na miwili. Juma ni mnyenyekevu shuleni, husumbuliwa na wanafunzi wenzake kwa sababu familia yake ni maskini. Jambo Hilo halimfurahishi hata kidogo.

Katika gwaride, Juma alitumwa nyumbani kwa sababu wavyele wake hawakuweza kulipa karo. Alikuwa na machozi wanafunzi wengine wakimcheka. Pia kuna mwanafunzi mwingine aliyeitwa Kamau,yeye ni mpole kama njiwa lakini hawezi pita mtihani. Hilo jambo linamkasirisha sana.

Siku Moja Juma aliona Kamau akisoma. Kamau alimweleza kuhusu shida yake. Juma aliamua kumsaidia na masomo. Ilikuwa ngumu, lakini aliendelea kumsaidia. Siku ya mtihani ilifika na Kamau alipita mitihani yote za muhula huo. Alijawa na furaha. Wazazi wake waliona ameanza kutia bidii kwa mitihani na walipomuuliza akawaambia kuhusu Juma. Wazazi wa Kamau walimtembelea Juma na wakampa zawadi kubwa. 

Hilo linamaanisha kwa ukweli wema hauozi.


David (12yrs) 

Mwanafunzi  kutoka kaunti  la Nairobi.

Januari .25 . 2025 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *