SAFARI NDOTONI
Ilikuwa siku ya ijumaa, tulienda kulala saa saba ya usiku. Nilijitaiyarisha kuingia kwa kitanda halafu mama alinitakia ndoto njema na nikamjibu,“yamafanikio.”
Nilianza kuota nikiwa katika ndege. Hilo ndege lilikuwa na watu wengi sana. Walikuwa wanakula chakula na wengine walikuwa wanaongea.
Tulishuka katika ndege na kuelekea kwa hoteli. Ilikuwa kubwa sana. Nikitembea niliona meli na nikaipanda. Meli hiyo ilisafiri kwa dakika mingi sana lakini nianza kula peremende na biskuiti.
Tulishuka kwa meli na kutembea mstuni. Niliona wanyama wengi kama nyati,nyoka,kiboko na Simba. Nilipopitia shambani nilimuona fisi na nikapiga nduru. Fisi alipo bweka, nami nikaanza kukimbia. Nilianza kucheka vile nilipompoteza fisi.
Mama alishtuka na kuniamsha kwa mashangao aliposkia nikipiga nduru. Nilimwambia kuhusu ndoto yangu, akasema kuwa hiyo ni ndoto ya usafiri.
Hiyo ndoto ilinifurahisha sana. Nilitamani sana kusafiri mahali na ndege au meli.
Amalia (10yrs)
Mwanafunzi kutoka kaunti la Nairobi.
Januari .25 . 2025