Africa Kids Book Club

WEMA HAUOZI

Nilikuwa natembea barabarani nikielekea mahojiano ya kuingia chuo kikuu cha wanafunzi wa fomula moja,nikakutana na mzee aliyehitaji usaidizi wangu kutengeneza gari lake. Mimi kuwa nimesomea uhandisi wa mitambo,nikaamua kumsaidia mzee huyo.

‘Shikamoo mzee, unaonekana unahitaji usaidizi kutengeneza gari lako?” nikamuuliza.

“Marahaba mwanangu, Ndio! Tafadhali nisaidie kutengeneza gari langu.Nimechelewa kuwahoji wanafunzi wangu.” Mzee akajibu.

Nilijua nitachelewa Mahojiano, lakini nilijiambia moyoni, wema hauozi.

Nilimuulizia funguo zake za gari na kuingia kujaribu kuwakisha gari,lakini haikuwaka.

“Oh! Nimeona shinda na gari lako, sio shinda kubwa sana, ni mafuta ya gari imeisha. Ukonayo kwa sasa?” Nikamuuliza.

“Naam! Wacha nichukue.” Mzee akajibu

Kutoka hapo niliweka mafuta kwa gari na kuiwasha. Lo! Gari likawaka!.

“Heko! Umetengeneza gari yangu. Asante sana mwanangu.” Mzee alinishukuru.

“Karibu sana. Wacha mimi nielekee mahojiano.” Nikamjibu

“La! Ingia kwa gari nikupeleke huko.” Mzee akanielekeza.

“Nashukuru sana lakini sikukusaidia ndio unirudishie usaidizi.” Nikajibu.

“La mwanangu,ingia kwenye gari nikupeleke mahojiano.”

Niliingia kwenye gari lake na tukaelekea. Nilimshukuru sana.

“Mbona umechelewa hivi?” Mhoji aliuliza

“Pole sana, nilikuwa ninamsaidia mzee aliyekuwa na shida ya gari”. Nilijibu.

“Sawa, basi Keti.” Mhoji akanielekeza

Niliketi kwenye kiti hicho na kugojea maswali ya mahojiano lakini nikamsikia mtu akibisha mlango.

‘Ingia!’ Mhoji akasema.

Mzee yule akaingia na kumsalimu mhoji.

“Mzee Nawiri! Umefika! Ndiiye huyu kijana ulikuwa umhoji!” Mhoji alishangaa.

“Oh! Ngojea! Ndiye huyu? Huyu ndiye amenisaidia kutengeneza gari!” Alisema kwa mshangao.

“Oh! Basi mpe darasa! Yeye ni mfano wa  watu tunaotafuta!’ Mzee akasema.

Nilipomskia akisema hivyo,nilishtuka sana. Mimi? hatahawajaniuliza maswali!

“Naomi,tumekuchagua uwe wanafunzi wa shule yetu.” Mjohi akanieleza

“Wah! Asante sana. “ Nikasema.

Ndio kwa kweli, wema hauozi.


Catherine (12yrs) 

Mwanafunzi  kutoka kaunti  la Nairobi.

Januari .25 . 2025

 

7 Responses

  1. We are very proud of you Cate. Seeing you write in Kiswahili is very encouraging knowing how much you struggled before – this is especially encouraging to those who are struggling

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *