Africa Kids Book Club

NDOTO YANGU

Ilikuwa usiku na nilikuwa tayari kulala. Nilipiga mswaki na kuelekea kwenye chumba cha kulala. Mama alinifunika na kusema, “lala unono mwanagu”. Nilifunga macho na nikasinzia.

Nilianza kuota nikiwa na ndugu na marafiki wangu tukicheza mpira wa miguu. Tulikuwa tumefunga mabao mawili kwa nunge. 

Wakati tuilipomaliza tuliona tumeitwa na  mama yangu. Tulipofika nyumbani tulipata mama amepika keki kubwa. Nilifurahi sana na nikaanza kupaa angani. Kila mtu alikuwa ameshangaa. Walianza kuruka juu ili wanivute chini lakini hawakuweza na nikapaa mpaka msitu. Kwa ghafla nikaanza kushuka pole pole.

Nilipofika chini nilimuona simba. Simba alianza kunifukuza. ilikimbia lakini simba alikuwa na mbio zaidi. Alienda kunikamata lakini nilipata mbio na nikamuacha nyuma. 

Nilipokimbia mbele kidogo nilipata njia na nikaamua kuifuata, niliona mama na baba wakiwa wananitafuta ili waninusuru. Nilikaribishawa nyumbani na peremende na keki. 

Kwa kweli ilikuwa ndoto ambayo sitasahau.


Roman (10yrs) 

Mwanafunzi  kutoka kaunti  la Nanyuki.

Februari .1 . 2025

 

4 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *